• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Reli ya Chengdu-Ulaya yaleta urahisi kwa usafirishaji wa bidhaa mjini Chengdu

  (GMT+08:00) 2017-07-03 17:02:21

   

  Kwenye mji wa Chengdu mkoani Sichuan, kuna duka moja liitwalo "Rong'ou Hui". Ukiingia kwenye duka hilo, utajiona kama uko kwenye supermarket barani Ulaya, ambapo bidhaa mbalimbali za kutoka Ulaya zinauzwa huko. Lakini ni kwa nini duka hilo linauza bidhaa zote zilizoagizwa kutoka Ulaya?

  Mkurugenzi wa duka hilo Bibi Shi Min amesema duka hilo lilizinduliwa mwezi Novemba mwaka 2016, na bidhaa zote zilisafirishwa kwa reli ya Chengdu-Ulaya, ambazo ni pamoja na vyakula, pombe na bidhaa za kutunza ngozi kutoka Ufaransa, Italia, Ujerumani n.k. Amesema bidhaa zinazouzwa na duka lake zina sifa nzuri na bei zake ni za chini.

  Duka hilo liko kwenye eneo la biashara nje la bandari ya reli ya kimataifa mjini Chengdu, ambapo bidhaa zote zilizosafirishwa na reli ya Chengdu-Ulaya zinauzwa hapa. Raia wa kawaida wanaweza kunufaika na urahisi ulioletwa na reli hiyo inayounganisha mji wa Chengdu na Ulaya.

  Mwezi Aprili mwaka 2013, treni ya kwanza ya reli ya Chengdu-Ulaya ilifunga safari kutoka Chengdu. Tarehe 20 mwezi Juni mwaka 2016, rais Xi Jinping wa China alishiriki kwenye sherehe ya kuzindua safari kutoka Chengdu hadi Poland. Hivi sasa kwa kupitia reli hiyo, wachina wanaweza kwenda Poland, Uturuki na Russia.

  Baada ya maendeleo ya kasi ya miaka kadhaa, reli ya Chengdu-Ulaya imetoa mpango rahisi zaidi wa usafirishaji wa bidhaa kwa kampuni za China na Ulaya. Wakati huo huo reli hiyo pia imehimiza ongezeko la usafrishaji wa bidhaa nje na uhamiaji wa viwanda. Mkurugenzi wa kampuni ya bandari ya reli ya kimataifa ya Chengdu anayeshughulikia uuzaji na soko Bibi. Zheng Shuangli amesema,

  "Kabla ya kuzinduliwa kwa reli ya Chengdu-Ulaya, kampuni na wafanyakazi wa Chengdu hawakuwa na imani na njia za kufanya biashara au kuagiza bidhaa barani Ulaya. Lakini hivi sasa kampuni nyingi zikiwemo kampuni ndogo zimeanza kufanya biashara na upande wa Ulaya, kwa sababu zimeona urahisi ulioletwa na reli ya Chengdu-Ulaya. Wakati huo huo, kuzinduliwa kwa reli hiyo pia kumehimiza uhamiaji wa baadhi ya viwanda mjini Chengdu. Kampuni maarufu zikiwemo TCL na Lenovo zimeanza kuzingatia kuanzisha vituo vya uzalishaji huko Chengdu. Tunaona kuwa usafirishaji wa bidhaa, biashara na viwanda vinaendelezwa kwa uwiano."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako