• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika inatafuta uhuru zaidi kwa mageuzi ya kuchangisha fedha

    (GMT+08:00) 2017-07-04 08:52:10

    Viongozi wa nchi za Afrika wanaohudhuria mkutano wa kilele wa 29 wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa wamepiga hatua zaidi kuwa na Umoja wa Afrika unaojitegemea kifedha.

    Rais Mugabe ambaye hapo awali aliahidi kuchangia ng'ombe 300 kwa ajili ya mfuko wa Umoja wa Afrika, amesema ni hadi viongozi wa Afrika watakapotambua majukumu yao, ndio umoja wa Afrika utakuwa wa waafrika kihalisi. Amesema kutafuta vyanzo mbadala vya fedha ni jukumu la dharura kwa umoja wa Afrika.

    Uamuzi wa umoja wa Afrika kujitegemea kifedha ulifikiwa kwenye mkutano wa 27 wa Umoja wa Afrika. Uamuzi huo unaitaka kila nchi mwanachama kuchangia asilimia 0.2 ya kodi ya uagizaji bidhaa kwa ajili ya Umoja wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako