• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuunga mkono ujenzi wa uwezo wa amani na usalama barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-07-04 09:43:24

    Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi jana huko New York amesema, mwezi Julai China itakuwa mwenyekiti wa zamu wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ambapo baraza la hilo litaendesha mikutano karibu 30 na mikutano miwili ya mjadala. Amesema mbali na mjadala kuhusu suala la Palestina na Israel, pia kutakuwa na mjadala kuhusu kuimarisha ujenzi wa uwezo wa amani na usalama barani Afrika.

    Bw. Liu Jieyi amesema mjadala huo unaweza kuweka mazingira ya baraza kufuatilia suala la amani na usalama barani Afrika, kuhimiza jumuiya ya kimataifa kuongeza ufuatiliaji kwa Afrika, na kuusaidia Umoja wa Afrika na nchi za Afrika kuimarisha ujenzi wa uwezo wa amani na usalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako