• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 14 wa Al-Shabaab wauawa Somalia

    (GMT+08:00) 2017-07-04 10:04:48

    Kamanda wa jeshi la serikali ya Somalia Bw. Mohamed Abdow Ali amesema, wapiganaji 14 wa kundi la Al-Shabaab wameuawa na wengine 17 wamejeruhiwa kwenye mapambano na jeshi la taifa la Somalia likiungwa mkono na kikosi cha Umoja wa Afrika katika sehemu ya kusini ya nchi hiyo.

    Bw. Ali amesema jeshi la Somalia lilishambulia kituo cha kundi la Al-Shabaab kilichoko umbali wa kilomita 20 kutoka wilaya ya Garbaharey, na askari watatu wa jeshi la serikali waliuawa katika mapambano hayo.

    Pia amesema jeshi la serikali sasa linadhibiti eneo la mapambano, na kuongeza kuwa litaendelea kufanya operesheni kama hiyo dhidi ya kundi la Al-Shabaab.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako