• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutoa mafunzo ya kilimo cha kisasa cha mpunga kwa wakulima nchini Cote d'Ivoire

    (GMT+08:00) 2017-07-04 18:29:45

    Wajumbe 40 kutoka sekta ya kilmo cha mpunga nchini Cote d'Ivoire watapata mafunzo ya mwezi mmoja yatakayotolewa na wataalamu wa China mjini Abidjan.

    Naibu mkurugenzi wa kituo cha ushirikiano wa kiuchumi na nje cha wizara ya kilimo ya China Bw. Hu Yan'an amesema wataalamu hao watawafundisha wakulima wa Cote d'Ivoire kilimo cha kisasa cha mpunga, ikiwemo uzalishaji wa mbegu za mpunga, upandaji, usimamizi mashambani, uvunaji na utengenezaji kupitia mafunzo ya darasani na mashambani.

    Mkurugenzi wa idara ya mpunga ya wizara ya maendeleo ya kilimo na vijiji ya Cote d'Ivoire Bw. Yacouba Dembele amesema Cote d'Ivoire imetunga mpango wa kujitegemea katika uzalishaji wa nafaka ifikapo mwaka 2018. Amesema nchi yake inawakaribisha wataalamu wa China kutoa mafunzo tena nchini humo, na kuisaidia nchi yake kupata wataalam wengi zaidi wa kilimo cha mpunga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako