• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe atoa dola za Marekani milioni moja kwa Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2017-07-04 18:42:56

    Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametoa dola za Marekani milioni moja kwa Mfuko wa Umoja wa Afrika na kusema, Umoja huo una uwezo wa kutatua suala la fedha wenywe.

    Akihutubia mkutano wa 29 wa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika unaofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, rais Mugabe amesema, ingawa pesa hizo ni ndogo, lakini, imeonyesha kama nchi hizo zikichukua hatua, zinaweza kupata fedha za kutosha kuendesha kazi za Umoja huo.

    Rais Mugabe pia amesema, ingawa ni vigumu kuacha misaada ya kimataifa, lakini ni lazima nchi hizo zijitahidi ili kupata udhibiti wa kikamilifu wa Umoja huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako