• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:COMESA kuwekeza kwenye utafiti wa kuimarisha uchumi

    (GMT+08:00) 2017-07-04 20:27:43

    Watafiti na wataalam wa masuala ya kiuchumi katika nchi za Comesa wametoa mwito wa kuwepo kwa sheria ya utafiti wa kiuchumi ili kustawisha maendeleo.

    Zaidi ya watafiti 60 wanaowakilisha taasisi tofauti wamesema nchi wanachama wa Comesa zinatapaswa kufadhili utafiti katika uwiano wa biashara .

    Mwangi Gakunya afisa mkuu wa mawasiliano ya mashirika amesema watafanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Comesa baada ya utafiti kutekelezwa.

    Mradi wa utafiti unafadhiliwa na wakfu wa kuimarisha uchumi Afrika na tayari dola milioni 3 zimtolewa kwa ajili ya utekelezaji.

    Wataalamu hao wamesema matokeo ya utafiti huo yatatumika katika kufanya maamuzi muhimu ya nchi za Comesa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako