• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Wadau wa sekta ya uvuvi wabuni mbinu za maendeleo

    (GMT+08:00) 2017-07-04 20:28:11

    Wadau wa sekta ya uvuvi katika kaunti ya Lamu wamekutana kujadiliana hatua za kuboresha uvuvi nchini Kenya.

    Warsha hiyo imeandaliwa chini ya mpango wa kitaifa wa Blue economy ili kuboresha maisha ya mvuvi na kumwezesha kufikia hatua ya ujasiriamali.

    Zaidi ya wadau 500 wakiwemo wavuvi na wanachama wa vikundi vya uvuvi wamehudhuria kongamano hilo.

    Grace Mburu waziri wa uvuvi na maendeleo amesema ukosefu wa miundo msingi miongoni mwa wavuvi ndio chanzo kinacholemaza sekta hiyo.

    Serikali kuu na zile za kaunti sasa zitabuni mbinu ya kuwezesha wavuvi kutekeleza uvuvi wa biashara na kuwapatia fedha za usaidizi wa kufanya uvuvi wa teknolojia ya kisasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako