• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumo wa ligi kuu Zanzibar 2017/2018 kujulikana jumamosi

    (GMT+08:00) 2017-07-05 09:03:15

    Vilabu 28 ambavyo vimo kwenye mchakato wa upatikanaji timu 12 za ligi kuu soka ya Zanzibar msimu mpya wa 2017/2018 watakutana na kupanga mchakato mzima wa upatikanaji wa timu hizo 12 katika kikao kitakachofanyika jumamosi hii Julai 8 katika ukumbi wa mikutano wa uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.

    Haya yamekuja baada ya chama cha soka Zanzibar (ZFA) kuwa mwanachama wa 55 wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) ambapo agizo la CAF ni kuwa ligi kuu msimu ujao 2017/2018 zanzibar iwe na timu 12.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako