• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Libya lazishutumu nchi tatu za Kiarabu kuunga mkono ugaidi nchini Libya

    (GMT+08:00) 2017-07-05 09:46:53

    Msemaji wa jeshi la Libya Ahmed al-Mesmary amezishutumu Qatar, Sudan na Uturuki kwa kuunga mkono ugaidi nchini humo.

    Akiongea na wanahabari huko Cairo, msemaji huyo ameeleza kuwa Qatar imefanya uhalifu dhidi ya ubinadamu na kwamba ana nyaraka za ushahidi zinazoonesha kuhusika kwa nchi hizo tatu katika utoaji wa vifaa, na kusema ataziwasilisha kwa jumuiya ya kimataifa. Amesema wanachohitaji kwa jumuiya hiyo ni kuondoa vikwazo vya silaha vilivyowekwa dhidi ya jeshi la Libya ili kupambana na magaidi.

    Amefafanua kuwa jeshi lake limepata mafanikio na kudhibiti maeneo mengi ya Libya licha ya kwamba wanapambana na makundi manne makubwa ya kigaidi, yakiwemo IS, al-Qaida, Muslim Brotherhood na magenge ya uhalifu yanayomiliki silaha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako