• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtandao wa reli ya kasi wa Delta ya Mto Zhujiang wanufaisha wakazi

    (GMT+08:00) 2017-07-05 18:25:32

    Tangu miaka ya hivi karibuni mtandao wa reli ya kasi kwenye sehemu ya Delta ya Mto Zhujiang umekuwa ukikamilishwa siku hadi siku, hii si kama tu imeleta fursa kubwa kwa maendeleo ya huko, bali pia imeleta urahisi wa usafari kwa wakazi wa huko. Serikali ya mkoa wa Guangdong hivi karibuni iliweka lengo la kujenga reli ya kasi kwenye miji yote mkoani humo kabla ya mwaka 2020, kukamilika siku hadi siku kwa mtandao huo hakika kutawanufaisha zaidi wakazi.

    Zamani mfanyabiashara wa Shenzhen Bw. Guo alilazimika kusafiri kwenda kwenye miji mingine kwa ndege, kwa sababu reli haikuwa ya kisasa, na kasi ya treni ilikuwa ndogo, lakini hali hiyo sasa imebadilika. Anasema

    "Hivi sasa reli ya kasi inaendelezwa kwa kasi, hivi sasa nakwenda kwenye miji mingine kwa treni ya kasi. Naondoka asubuhi, na jioni naweza kurudi nyumbani, ni rahisi sana. Reli ya kasi imeleta urahisi mkubwa kwa kazi zangu."

    Maendeleo ya reli ya kasi si kama tu yameleta urahisi kwa watu wa miji ya Delta ya Mto Zhujiang na mkoa wa Guangdong, bali pia yameleta fursa nyingi zaidi za utalii kwa miji iliyoko kwenye kando za reli, hivyo yamehimiza maendeleo ya uchumi. Bw. Li anaishi kwenye mji wa Nanning mkoani Guangxi, alisema zamani kwenda mjini Guangzhou au mjini Shenzhen kulihitaji muda mrefu, lakini hivi sasa anakwenda Guangzhou kutoka Nanjing kwa saa tatu tu, hivyo ana fursa nyingi zaidi za kutalii mkoani Guangdong.

    Bw. Zhao anayefanya kazi mjini Shenzhen alisema, reli ya kasi imehimiza uhamiaji wa watu wenye ujuzi. Miji mikubwa ya kando ya reli ya kasi inavutia watu wenye ujuzi kutoka miji jirani. Alisema watu wa mikoa ya Hunan, Hubei na Guangxi wanakuja Guangzhou na Shenzhen kwa njia ya reli ya kasi kutoka kwao. Kujenga kwa reli ya kasi kumepanua eneo la watu kupata nafasi za ajira.

    Imefahamika kuwa reli ya kasi inayounganisha Guangzhou, Shenzhen na Hongkong inatarajiwa kuzinduliwa mwaka kesho. Baada ya kuzinduliwa kwa reli hiyo, watu kutoka Hongkong wataweza kufika Shenzhen kwa dakika 14, na kufika Guangzhou kwa dakika 48. Reli hiyo itafanya mawasiliano kati ya Hongkong na China bara yawe karibu zaidi.

    Kutokana na mpango husika wa mkoa wa Guangdong, katika siku za baadaye mkoa huo utaharakisha ujenzi wa mtandao wa reli ya kasi mkoani humo, kuhimiza ujenzi wa reli kati ya miji, na kutimiza lengo la kujenga reli ya kasi kwenye miji yote. Hakika maendeleo ya sehemu ya Delta ya Mto Zhujiang yatanufaishwa na reli ya kasi mkoani humo, na wakazi wa huko watapata urahisi zaidi kutokana na maendeleo ya reli ya kasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako