• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanajimu wa Marekani wagundua mashimo meusi mawili yanayozungukana

  (GMT+08:00) 2017-07-05 19:42:33

  Kituo cha taifa cha ufuatiliaji wa mawimbi ya radio toka angani cha Marekani hivi karibuni kimetoa taarifa kikisema wanajimu wakitumia darubini ya radio wamegundua mashimo meusi mawili makubwa yanayozungukana.

  Mashimo meusi hayo mawili yako katikati ya galaksi No. 0402+379 ambayo iko umbali wa miaka milioni 750 ya kusafiri kwa mwanga kutoka dunia yetu. Umbali kati ya mashimo hayo mawili ni miaka 24 ya kusafiri kwa mwanga, uzito wa jumla wa mashimo hayo ni mara bilioni 15 ya jua. Inakadiriwa kuwa inahitaji miaka elfu 30 kwa mashimo hayo kuzungukana kwa mzunguko mmoja.

  Shimo jeusi ni gimba la angani lenye mvuto mkubwa sana hata mwanga hauwezi kutoka, hivyo watu hawawezi kuona moja kwa moja shimo jeusi. Lakini shimo jeusi linapovuta vitu kutoka nje linatoa mawimbi makubwa ya radio, hivyo tunaweza kujua mahali lilipo shimo hili kupitia mawimbi hayo.

  Katika sehemu ya katikati ya galaksi nyingi ikiwemo galaksi yetu ya Milky Way, kuna mashimo meusi makubwa sana. Watafiti wamesema mashimo meusi mawili waliyoyaona yanatoka galaksi mbili zilizoungana pamoja, na inakadiriwa kuwa mashimo hayo yataungana pamoja mwishowe, na wakati yatakapoungana, yatatoa mawimbi makubwa ya mvuto ambayo yataathiri ulimwengu mzima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako