• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chris Bosh kuachana na timu Miami Heats baada ya kupata maradhi

    (GMT+08:00) 2017-07-06 09:36:43

    Baada ya muda wote wa miaka 13 aliochezea Miami Heats sasa Chris Bosh anaachana na timu hiyo na habari zinasema Bosh ameondolewa Miami Heats kutokana na ushauri wa madaktari baada ya kuonekana na tatizo katika mzunguko wa damu na kupelekea damu kuganda.

    Raisi wa Miami Heats Pat Rilley aliitangazia dunia na wapenzi wote wa kikapu haswa wa Miami Heats kwamba Bosh hataonekana tena katika timu hiyo na kwa kuheshimu hilo Miami Heats wameamua kustaafisha jezi yake namba 1 kama heshima kwa Bosh.

    Baada ya taarifa hiyo washkaji zake Bosh ambao ni Wade na Lebron hawakusita kuonesha hisia zao kupitia kurasa zao za Twitter ambapo kila mmoja aliandika ujumbe wa kumtakia kila la kheri Bosh katika maisha yake yajayo ya kikapu.

    Pamoja na Bosh kuondolewa na Miami Heats lakini klabu hiyo bado itaendelea kumlipa mchezaji huyo kwa muda wa miaka miwili ambapo atalipwa kiasi cha dola 52.1m.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako