Wateja nchini Uganda wamelalamikia riba ya juu inayotozwa na benki ya maendeleo nchini humo UDB.
Wanasena riba za benki hiyo bado ni za juu kukaribia zile za benki za kibiashara.
Kwa wastani riba za benki hiyo zimesalia kuwa kati ya 10 na 15 kwa kipindi cha miaka mitatu.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wakurungezi kwenye benki hiyo Samuel Sejjaka, hata hivyo amesema riba zao zinaendana na zile za kimataifa za benki za maendeleo.
Naye mkurungezi mkuu wa benki hiyo Patricia Ojangole, amesema riba hiyo ya juu inatokana na gharama kubwa za kufanya biashara.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |