• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Afrika Kusini lapinga hukumu ya mahakama ya kimataifa kuhusu suala la Rais wa Sudan

    (GMT+08:00) 2017-07-07 09:53:23

    Bunge la Afrika Kusini jana lilipinga hukumu iliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC, kuhusu Afrika Kusini kushindwa kutekeleza wajibu wake kwa mahakama hiyo na kumkamata Rais Omar Al Bashir alipokuwa nchini Afrika Kusini mwezi juni mwaka 2015.

    Msemaji wa kamati ya ushirikiano wa kimataifa ya bunge la Afrika Kusini Bw Shiphosezwe Masango, amesema inatakiwa kukumbwa kuwa Rais Al Bashir hakwenda Afrika Kusini kwa mwaliko wa serikali ya Afrika Kusini, bali alikuwa anahudhuria mkutano wa umoja wa Afrika.

    Amesema kama ilivyo kwa Umoja wa mataifa ambako marais wanahudhuria mikutano muhimu nchini Marekani, lakini hawawezi kukamatwa.

    Amesema kama ICC itaendelea na msimamo wake kuhusu hukumu hiyo, basi serikali ya Afrika Kusini italichukulia suala la kujitoa kwenye mahakama hiyo kama suala la haraka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako