• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yahitaji wafanyakazi zaidi ya elfu 7 wa afya kuziba pengo

    (GMT+08:00) 2017-07-07 10:38:29

    Maofisa wa matibabu wa kikanda nchini Tanzania wameiomba serikali kuwaajiri haraka wafanyakazi 7,304 wapya wa afya ili kuziba pengo lililoachwa na wafanyakazi waliofukuzwa kazini kutokana na vyeti feki.

    Mwenyekiti wa maofisa wa matibabu wa kikanda katika Tanzania Bara, Bw. Lenonard Subi amesema, wafanyakazi zaidi ya elfu 7 wanatakiwa kuajiriwa kabla ya hali ya hospitali kutoweza kudhibitiwa.

    Wafanyakazi 7,304 wa afya walifukuzwa kazini mwanzoni mwa mwaka baada ya kugunduliwa kupata ajira kwa kutumia vyeti feki na kusababisha ukosefu wa wafanyakazi kufikia asilimia 49.5.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako