• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Imetimia miaka 27 tangu jeshi la China lianze kushiriki kwenye operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa

  (GMT+08:00) 2017-07-07 16:21:14

  China ikiwa ni nchi inayotuma walinzi wa amani kwa wingi zaidi miongoni mwa nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa, kuanzia mwaka 1990 hadi sasa jeshi lake limeendelea kushiriki kwenye operesheni za kulinda amani katika nchi mbalimbali zenye migogoro duniani kwa miaka 27 mfululizo,.

  Hadi sasa jeshi la China kwa ujumla limetuma wanajeshi zaidi ya elfu 35 kushiriki kwenye operesheni 24 za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa, na kusifiwa na jumuiya ya kimataifa kuwa ni "nguvu muhimu katika operesheni za kulinda amani".

  Katika miaka 27 iliyopita, ushiriki wa jeshi la China kwenye operesheni za ulinzi wa amani umeendelea kupanuka, kutoka kushiriki kwenye operesheni moja hadi kushiriki kwenye operesheni nyingi kwenye mabara tofauti kwa wakati mmoja, kutoka kutuma askari wa uhandisi hadi kutuma wanajeshi wa vikosi mbalimbali, ambao mwanzoni walipewa hadhi ya waangalizi wa kijeshi, hadi sasa wanachukua nyadhifa mbalimbali kama vile wanadhimu na makamanda wa vikosi.

  Mwezi Septemba mwaka 2015, China ilitangaza kujiunga na utaratibu wa nguvu ya akiba ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa, na kuunda vikosi vya askari elfu nane kwa ajili ya operesheni za kulinda amani, ikiwa ni hatua ya kutekeleza ahadi yake ya kupanua ushiriki wake katika kulinda amani na usalama wa kimataifa, na kuonesha nia thabiti ya China kuunga mkono operesheni za Umoja wa Mataifa.

  Vurugu na ghasia, njaa na umaskini, joto na maradhi, bila kujali mazingira magumu na hatari kubwa, walinzi wa amani wametekeleza na kukamilisha majukumu ya kulinda amani waliyopewa kwenye maeneo tofauti duniani.

  Katika hali mpya ya kimataifa, walinzi wa amani wa China wameitikia mtizamo wa "Jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja", na kufungua kwa vitendo ukurasa mpya wa shughuli za kulinda amani za China.

  Wakati ushiriki wa jeshi la China kwenye operesheni za kulinda amani duniani unazidi kupanuliwa, sura ya askari wa China wenye udhati, urafiki, upendo, ushupavu na uwajibikaji inakubaliwa zaidi na watu wa nchi mbalimbali duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako