• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gambia yaunga mkono mageuzi ya Umoja wa Afrika ya kuwahusisha vijana

    (GMT+08:00) 2017-07-07 16:54:25

    Serikali ya Gambia imeeleza kuunga mkono ajenda ya mageuzi ya Umoja wa Afrika kuhusu kuboresha utawala bora kupitia kuwahusisha vijana wa bara la Afrika.

    Mkurugenzi wa mawasiliano na uhusiano wa umma wa Gambia Amie Bojang-Sissoho amesema, kaulimbiu ya kuchochea ongezeko la uchumi kupitia ongezeko la idadi ya watu na kuwekeza zaidi kwa vijana imekuja kwa wakati mwafaka katika kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa vijana, eneo ambalo limewekewa kipaumbele na serikali ya nchi hiyo.

    Pia amesema masuala mengine yanayolengwa kama amani na usalama pamoja na kutoa maisha ya baadaye ambayo ni salama kwa vijana wa Afrika kupitia mkakati wa kuwahusisha vijana pia vimehusishwa kwenye malengo ya serikali ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako