• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China azitaka nchi za BRICS kusaidia kufungua uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2017-07-07 19:26:33

    Rais Xi Jinping wa China amezitaka nchi wanachama wa BRICS kujenga bila kusita uchumi wa wazi wa dunia, kuongoza biashara ya pande nyingi, na kuboresha maendeleo ya pamoja.

    Rais Xi ametoa mapendekezo hayo katika mkutano usio rasmi wa viongozi wa nchi wanachama wa BRICS, kabla ya mkutano wa Kundi la nchi 20 (G20) unaofanyika mjini Hamburg, Ujerumani.

    Katika mkutano huo, viongozi wa BRICS wamebadilishana maoni kuhusu mazingira ya sasa ya kisiasa na kiuchumi duniani na vipaumbele vya G20, na kutoa makubaliano muhimu kuhusu kuimarisha umoja na uratibu wa BRICS.

    Rais Xi, ambaye aliongoza mkutano huo, pia alitoa wito kwa nchi wanachama wa kundi hilo kusukuma mbele utatuzi wa amani wa migogoro na mivutano ya kikanda na kutumia vema mfumo wa G20 kama jukwaa la mwanzo kwa ushirikiano wa kimataifa wa kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako