• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Marekani, Japan na Korea Kusini watoa taarifa ya pamoja kuhusu suala la nyuklia la Peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2017-07-08 18:40:08

    Rais Donald Trump wa Marekani, rais Moon Jae-in wa Korea Kusini na waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe katika kipindi cha mkutano wa kilele wa kundi la nchi 20 unaoendelea huko Hamburg walifanya mazungumzo kuhusu suala la nyuklia la Peninsula ya Korea na kutoa taarifa ya pamoja kuilaani Korea Kaskazini kufanya jaribio la kurusha makombora ya masafa marefu.

    Taarifa imesema kuwa, kufanya jaribio la kurusha makombora kulikwenda kinyume na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na pia ni uchochezi kwa nchi hizo tatu na nchi nyingine duniani. Viongozi wa nchi hizo tatu walisisitiza uhumimu wa kushirikiana kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea na kusisitiza kutimiza lengo la kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye peninsula kwa njia ya amani. Nchi hizo tatu zitashirikiana kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo na kuanzisha tena mazungumzo kuhusu kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye pPeninsula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako