• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa yataka ulinzi kwa watoto wa Sudan Kusini baada ya miaka 6 ya mateso

    (GMT+08:00) 2017-07-09 19:37:55
    Umoja wa Mataifa yataka ulinzi kwa watoto wa Sudan Kusini baada ya miaka 6 ya mateso.

    Mfuko wa watoto na Shirika la kuhudumia watoto (UNICEF) jumamosi limetaka kuimarishwa ulinzi kwa watoto kabla ya kumbukumbu ya miaka sita ya Uhuru wa Sudan Kusini.

    Katika taarifa iliyotolewa mjini Juba, UNICEF ilisema matumaini na ndoto kwa watoto wa taifa hilo changa bado hazifanywi kwa vitendo, na kuelezea hali ya nchi hiyo kama janga la watoto.

    Muwakilishi wa UNICEF Sudan Kusini Mahimbo Mdoe ameeleza kuwa zaidi ya watoto 2000 wameuawa au kujeruhiwa, na wengi zaidi wameshuhudia vurugu mbaya. Idadi hiyo ni kubwa na bado kila inawakilisha mateso yanayoendelea ya mtoto.

    Sudan Kusini inaongoza kwa kiwango cha juu duniani kwa watoto kutohudhuria shule, na zaidi ya asilimia 70 ya watoto hawapati elimu huku zaidi ya theluthi moja ya shule zote zimeshambuliwa na vikundi vyenye silaha.

    Kwa mujibu wa UNICEF, kuharibika kwa mifumo ya afya, maji na usafi wa mazingira Sudan Kusini, ni chanzo cha watoto kupoteza maisha kutokana na kukumbwa na magonjwa kama vile kipindupindu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako