• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Malinzi ajiuzulu uongozi FIFA

    (GMT+08:00) 2017-07-10 08:55:27
    Rais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi amejiuzulu wadhifa wake wa ujumbe wa kamati ya maendeleo ya Shirikisho la soka la kimataifa (FIFA).

    Kupitia kwa wakili wake, Malinzi amewaandikia barua FIFA kuwataarifu kujitoa kwenye kamati hiyo kutokana na kuwa mikononi mwa sheria kwa sasa.

    Malinzi pamoja na katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa na mhasibu Nsiande Isawafo Mwanga wapo rumande hadi Julai 17, upelelezi wa kesi yao utakapokamilika baada ya kunyimwa dhamana Julai 3 katika kesi inayowakabili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako