• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makubaliano ya kusimamisha vita kusini magharibi mwa Syria yaanza kufanya kazi

    (GMT+08:00) 2017-07-10 09:52:04

    Makubaliano ya kusimamisha vita katika meneo ya kusini magharibi mwa Syria yaliyofikiwa kati ya Marekani, Russia na Jordan yameanza kutekelezwa rasmi tangu jana.

    Mpaka sasa jeshi la serikali ya Syria na makundi ya upinzani yanaendelea kuheshimu makubaliano hayo. Lakini kutokana na baadhi ya maeneo yaliyotajwa kwenye makubaliano hayo kuwa chini ya udhibiti wa kundi la IS, utekelezaji wa usitishaji vita unakabiliwa na changamoto na hali zisizotabirika.

    Habari zinasema Marekani, Russia na Jordan zilifikia makubaliano hayo ili kusaidia kukomesha uhasama na kurejesha utulivu kusini magharibi mwa Syria na kuwezesha usambazaji wa misaada ya kibinadamu kwenye maeneo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako