• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu wa Iraq ataka jeshi lihakikishe usalama wa mji wa Mosul

    (GMT+08:00) 2017-07-10 09:58:19

    Waziri Mkuu wa Iraq Bw Hader al Abadi amelitaka jeshi la Iraq kuwatokomeza wapiganaji wa kundi la IS, na kuhakikisha usalama wa mji wa Mosul.

    Bw Abadi ametoa amri hiyo alipokutana na makamanda wa jeshi la Iraq baada ya kuwasili mjini Mosul, na kuwapongeza kutokana na ushindi wa kuukomboa mji huo kutoka kwa wapiganaji wa kundi la IS.

    Ameliamuru jeshi kuondoa mabomu yote ya kutegwa ardhini na kuwalinda rais wote waliopoteza makazi.

    Maofisa wa jeshi la Iran pia wameipongeza Iraq kwa kuukomboa mji wa Mosul. Waziri wa Ulinzi wa Iran Bw Hussien Dehqan amesema kushinda na kutokomeza ugaidi kutawezekana kutokana na dhamira kamili ya serikali kupambana na ugaidi kwa ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako