• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Kenya atoka hospitali

    (GMT+08:00) 2017-07-10 19:14:02

    Mgombea urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya Bw. Raila Odinga ametoka hospitali huko Mombasa jana usiku.

    Mshauri wake Bw. Salim Lone amesema, waziri mkuu huyo wa zamani anayeongoza Muungano wa vyama vya Upinzani wa NASA atafanyiwa vipimo zaidi jijini Nairobi baada ya kupata tiba kwa saa kadhaa huko Mombasa, na kwamba mpaka asubuhi ya leo Bw. Odinga alikuwa anaendelea vizuri.

    Kiongozi huyo wa upinzani alikimbizwa hospitalini baada ya kuhutubia mikutano kadhaa ya kisiasa huko Mombasa. Baada ya kutoka hospitali, Bw. Odinga amesema kuwa afya yake ni nzuri, na kwamba atakwenda jijini Nairobi kwa ajili ya kuendelea na kampeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako