• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wakulima wamefaidika na bei ya miwa yao kuongezeka hadi Sh4,300

    (GMT+08:00) 2017-07-10 20:00:30

    Wakulima wameibuka washindi baada ya maafisa kuongezeka gharama ambayo wasagaji wananunua nayo miwa hadi Sh4,300 kwa tani, jambo ambalo limeingiza shinikizo kwenye viwanda vilivyomilikiwa na serikali.

    Bei mpya ni Sh500 zaidi ya Sh3,800 ambayo wasagaji wamekuwa wakilipa wakulima tangu Oktoba.

    Bei ya juu inangaliwa kupandisha gharama ya kuzalisha sukari ya ndani na zaidi kupunguza ushindani wa viwanda vya ndani dhidi ya bidhaa za bei nafuu.

    Maeneo mengi ya uzalishaji sukari nchini yanakabiliwa na uhaba mkubwa ambao unachangiwa na ukame ulioathiri maeneo hayo.

    Bodi ya Sukari imesema katika kipindi cha Januari hadi Aprili mwaka 2017, uzalishaji wa bidhaa ulishuka hadi tani 172,722 ikilinganishwa na tani 238,872 zilizopatikana katika kipindi hicho mwaka jana.

    Kenya inazalisha tani 600,000 za sukari kila mwaka na inategemea uagizaji ili kukidhi mahitaji ambayo sasa yanasimama 900,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako