• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yategemea kufufua tena uchumi kupitia mradi mpya wa SGR

    (GMT+08:00) 2017-07-11 19:16:29

    Mradi wa treni ya SGR kati ya Nairobi na Naivasha ambao ulizinduliwa rasmi mwaka jana utafungua njia kwa shughuli nyingi za kibiashara katika njia yake.

    Waziri wa uchukuzi na miundombinu wa Kenya James Macharia amesema kuwa, reli hiyo ya kisasa itafungua maeneo ya ndani ya Kenya kwa ajili ya uwekezaji. Amesema faida ya kiuchumi ya reli hiyo inatarajiwa kuongezeka kutokana na ujenzi unaoendelea kutoka Nairobi hadi Naivasha na hatimaye Kisumu na Malaba.

    Oktoba 19 mwaka jana, rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alizindua ujenzi wa awamu ya pili ya mradi wa reli ya Nairobi hadi Naivasha unaofadhiliwa na China na wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.5.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako