• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Kenya kuanza safari za moja kwa moja hadi Marekani mwaka 2018

  (GMT+08:00) 2017-07-11 19:19:54

  Kikao cha hivi karibuni baina ya halmashauri ya safari za ndege nchini Kenya na ile ya Marekani kimebainisha kwamba huenda Kenya itaidhinishwa kuanzisha safari za moja kwa moja hadi Marekani mwaka ujao.

  Mwenyekiti wa halmashauri ya masuala ya safari za angani nchini Kenya mhandisi Nkadayo amesema Kenya itakuwa miongoni mwa nchi nyingine 5 pekee zilizopewa wadhfa huo Afrika.

  Kulingana na mwenyekiti huyo,hatua ya pili itahusisha kampuni zote za ndege zinazotaka kusafiri hadi Marekani kufanyiwa ukaguzi .

  Utaratibu kamili utafanyika mwezi Oktoba mwaka huu kabla ya kujadiliwa Marekani na kwa miezi minne ijayo .

  Kampuni ya Kenya Airways inatarajiwa kuwa kampuni ya kwanza kuidhinishwa baada ya ukaguzi na huenda ikaanza safari hizo mwaka 2018 .

  James Macharia waziri wa uchukuzi Kenya amesema safari hizo zitafungua fursa za biashara na kuvutia watalii na wawekezaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako