• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda:Wataalamu wasaka sheria ya kudhibiti sarafu ya dijitali Uganda

  (GMT+08:00) 2017-07-11 19:20:29

  Idara ya polisi na wataalamu wa masuala ya fedha Uganda wanataka kuwepo kwa sheria ya kudhibiti sarafu za dijitali zinazojulikana kama Crypto ili kuzuia visa vya udanganyifu wa elektroniki.

  Dan Munanura kamishena wa kitengo cha elktroniki kwenye idara ya polisi Uganda amesema sarafu za dijitali za crypto zimechangia utengenezaji wa fedha bandia na pia wateja kuibiwa fedha kwa njia ya dijitali.

  Idara ya polisi sasa imeanzisha uchunguzi wa sarafu hiyo inayoendeshwa na watu wasiojulikana katika mtandao.

  Upande wa wawekezaji wa fedha hizo za dijitali,wamelalama kwamba pendekezo la kusimamisha ama kudhibiti sarafu hiyo litawapatia hasara.

  Sio Crypto pekee katika miaka ya hivi karibuni sarafu za bitcoins zimevutia baadhi ya wafanyibiashara.

  Benki kuu ya Uganda imwatahadharisha waganda dhidi ya udanganyifu huo na kuwataka kuripoti hali zozote za utata.

  Mwkaa 2016 zaidi ya shilingi bilioni 20 zilipotea kupitia huduma za fedha za dijitali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako