• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Wakulima waiomba serikali kupunguza bei ya vyakula vya mifugo

    (GMT+08:00) 2017-07-11 19:20:49

    Wafugaji nchini Rwanda wameitaka serikali ya nchi hiyo kupunguza bei ya vyakula vya mifugo wao ili kupunguza gharama ya biashara.

    Hali hii imejitokeza kufuatia mapato duni ya chini ya asilimia 60 katika kilimo cha mifugo.

    Wakulima hao chini ya muungano wa chama cha mifugo wamelazimika kuchanganya vyakula vya madukani na vile vya kienyeji ili kufikia malengo yao jambo ambalo limepelekea kushuka kwa uzalishaji.

    Manasseh Ngahabwa afisa mkuu wa idara ya lishe bora ya wanyama ,amethibitisha ongezeko la bei ya chakula kutoka franki 200 hadi 359 kwa kilo.

    Aidha katika maduka mengine chakula cha kuku kimepanda hadi franki 380 kilo kutoka 180 mwaka jana.

    Vital Hategekimana mfugaji wa kuku wa biashara analalama kwamba hutumia franki 33,000 kwa siku ili kununua kilo 100 za chakula cha kuku wake 2000 ambay ni zaidi ya ongezeko la asilimia 60 ya gharama zake.

    Hata hivyo Fabrice Ndayisenga mkurugenzi wa bodi ya kilimo ameitetea serikali akisema kwamba waliongeza ushuru latika vyakula vya wanyama ili kuimarisha sekta ya viwanda vya kuzalisha na kutengeneza bidhaa hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako