• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanajeshi wa AU wakabidhi chuo kikuu cha taifa kilichotumika kama kambi ya jeshi

    (GMT+08:00) 2017-07-12 09:53:06

    Wanajeshi wa Burundi walio chini ya Tume ya Umoja wa Afrika AMISOM jana waliondoka kutoka chuo kikuu cha taifa ambacho kimekuwa kambi kubwa ya tume hiyo iliyotumika kwa miaka 10.

    Kwenye taarifa yake AMISOM imesema wanajeshi 300 waliokuwa kwenye Chuo Kikuu cha Taifa wamehamishiwa kwenye kambi ya AU ya Jowhar kuanzia mwaka jana. Mwakilishi maalumu wa AU nchini Somalia Bw Francisco Madeira amesema hatua hiyo ni maendeleo yaliyofikiwa na AMISOM na serikali, katika juhudi za kulidhibiti kundi la Al-Shabaab, kuleta utulivu, kufanya maisha yawe ya kawaida, na kuendeleza nchi.

    Wanajeshi wa Burundi walianza kuwepo kwenye chuo hicho mwaka 2007 ambapo ilianza kama kambi ndogo, na baadaye kuwa makao makuu ya Batalioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako