Wizara ya ulinzi ya Uturuki imesema zaidi ya wanajeshi elfu saba wakiwemo majenerali 150, wamefukuzwa kazi kwa tuhuma za kushirikiana na kundi linaloongozwa na Fethullah Gulen. Serikali ya Uturuki imemshutumu kiongozi wa kidini Fethullah Gulen anayeishi Marekani, kuwa mpangaji wa jaribio lililoshindwa la mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea Julai 15 mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 250, na kuliorodhesha kundi la Gulen kuwa kundi la kigaidi. Mpaka sasa watu wapatao laki 1.1 wamefutwa kazi serikalini kwa kuhusika na mapinduzi hayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |