• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la Boko Haram laendeleza mashambulizi yake Nigeria

    (GMT+08:00) 2017-07-13 09:09:20

    Hali katika mji wa Maiduguri nchini Nigeria bado inaendelea kuwa tete baada ya wapiganaji waliobaki wa kundi la Boko Haram kufanya mashambulizi wiki iliyopita.

    Seneta wa jimbo la Borno Bw Ali Ndume amesema hali kwa sasa inatia wasiwasi na kuwataka wananchi kuungana kuliangamiza kundi hilo. Mji wa Maiduguri umekuwa ukikumbwa na mashambulizi mfululizo, likiwemo lile la Chuo kikuu cha Maiduguri ambapo watu kadhaa waliuawa akiwemo profesa mmoja.

    Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari mwaka huu wapiganaji wa Boko Haram wamefanya zaidi ya mashambulizi 40 yaliyosababisha vifo vya raia wengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako