Wanachama wote 83 wa kamati hiyo waliokutana kwa kikao cha 130, walipiga kura kuunga mkono uamuzi uliofanywa na bodi ya IOC mwezi uliopita.
Miji ya Los Angeles and Paris yalikuwa wawaniaji pekee walioweka maombi ya kuandaa michezo ya Olimpiki mwaka wa 2024 baada ya miji kadhaa zikiwemo Oslo, Roma, Budapest na Munich kujiondoa.
Mwenyeji wa michezo hiyo ataamuliwa kwa kura itakayofanyika septemba 13 kwenye mji wa Lima nchini Peru, kwenye kikao cha 131 cha IOC.
Meya wa Los Angeles Eric Garcetti na mwenzake wa Paris Anne Hildago waliungana jukwaani na kushikana mikono wakiwa pamoja na rais wa IOC Thomas Bach kwa ishara ya umoja na kusherehekea uamuzi huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |