• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema kitendo cha India kuvuka mpaka wa China safari hii ni tofauti na mikwaruzano ya zamani

    (GMT+08:00) 2017-07-13 09:34:39

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, kitendo cha jeshi la India kuvuka mpaka wa Sikkim unaotambuliwa kwa pamoja na China na India na kuingia kwenye ardhi ya China safari hii kina tofauti za kimsingi na mikwaruzano ya zamani ambayo ilitokea kwenye maeneo ya mpaka wenye mgogoro kati ya nchi hizo mbili.

    Bw. Geng Shuang amesema, mpaka wa Sikkim ni mpaka pekee uliokubaliwa na pande zote mbili za China na India, ambao ni tofauti kabisa na mipaka ya Mashariki, Kati na Magharibi isiyothibitishwa rasmi. Mkataba wa China na Uingereza kuhusu Tibet na India uliosainiwa mwaka 1890 uliweka rasmi mpaka wa Sikkim, ambao uhalali wake unatambuliwa na serikali za China na India. Bw. Geng Shuang amesisitiza kuwa China inaitaka India kwa mara nyingine irudishe mara moja vikosi vyake kutoka kwenye ardhi ya China bila masharti, na kutatua tukio hilo kwa hatua mwafaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako