• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Huang Danian:Mwanasayansi wa China, mzalendo wa kweli

    (GMT+08:00) 2017-07-13 14:49:25

    Mwanasayansi maarufu wa jiofikizia wa China Bw. Huang Danian alifariki dunia Januari 8 mwaka huu, akiwa na umri wa miaka 58. Katika maisha yake mazima Bw. Huang alijitolea nguvu na akili zote kwenye utafiti wake na kuonesha uzalendo kwa taifa.

    Kabla ya kuanza utafiti wake nchini China, Bw. Huang alisoma shahada la uzamivu nchini Uingereza na kuwa mkurugenzi wa kitengo cha utafiti cha kampuni ya jiofikizia ya Arkex iliyoko chini ya Chuo kikuu cha Cambridge. Alipoulizwa kwa nini aliacha wadhifa wake wenye mapato makubwa na kuamua kurudi nyumbani China, alisema ni bahati nzuri kwake kupata fursa ya kutoka nje kujiendeleza kimasomo, na pia ni lazima kwake kurudi nyumbani na ujuzi aliopata kulitumikia taifa.

    Mwaka 2009 Bw. Huang alirudi China, na mara moja alianza kazi za utafiti kwenye kitivo cha jiografia cha Chuo kikuu cha Jiling. Katibu wake Wang Yuhan alisema Bw. Huang alikuwa akifanya kazi mpaka saa nane au tisa alfajiri, na kama ukiona taa za ofisi yake zimezimwa, basi ina maana amesafiri kikazi. Amesema kwa wastani theluthi moja ya kila mwaka Bw. Huang huwa yuko kwenye safari za kikazi katika sehemu mbalimbali nchini, ambazo anasema zimesaidia kuelekeza utafiti wa jiofizikia wa China kwenye njia sahihi katika siku zijazo.

    Moja ya vipaumbele kwenye utafiti wa Bw. Huang ni kusanifu na kutengeneza zana ya "gravity gradiometer" yenye usahihi wa hali ya juu, ambayo ni muhimu katika kutafuta mafuta na madini, na pia inaweza kutumika katika nyambizi kwa malengo ya kijeshi. Msaidizi wake profesa Yu Ping amesema Bw. Huang alishirikisha taasisi zaidi ya kumi na mamia ya watafiti kwenye utafiti huo, na kutumia muda wa miaka mitano kuboresha uwezo wa zana hiyo wa kukusanya data na kuinua usahihi wake kufikia kiwango cha kimataifa.

    Wakati wa kuhitimu kutoka chuo cha jiolojia cha Changchun, Bw. Huang Danian aliandika kwenye kumbukumbu ya wahitimu kuwa "Ni wajibu wetu kustawisha taifa la China". Huo ndio moyo wa uzalendo uliomhimiza Bw. Huang kujitolea kwa nguvu zote kwenye kazi za utafiti, hata wakati alipogunduliwa kuwa na saratani na kulazwa.

    Siku moja kabla ya kufanyiwa upasuaji wa mwisho, Bw. Huang pia alikwenda kufanya kazi ofisini na ilikuwa mara yake ya mwisho kuingia ofisi yake.

    Ingawa Bw. Huang amefariki dunia, lakini utafiti alioongoza bado unaendelea. Wenzao wake wanajitahidi kuendeleza nadharia yake kwa ajili ya matumizi halisi, ili kukamilisha ndoto yake isiyotimizwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako