• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya ulinzi ya Marekani yasema jeshi lake limeingia katika makao makuu ya kundi la IS nchini Syria

    (GMT+08:00) 2017-07-13 17:51:37

    Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Bw. Ryan Dillon amesema, jeshi la nchi hiyo limeingia katika makao makuu ya kundi la IS huko Ar Raqqah nchini Syria, na kusaidia makundi ya silaha ya huko kupambana na kundi la IS.

    Bw. Dillon amesema, jukumu la jeshi hilo pamoja na jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani ni pamoja na kutoa ombi la uungaji mkono kutoka anga kufuatia hali ya ardhini.

    Juni 6 kundi la SDF linaloungwa mkono na jeshi la Marekani lilianza kufanya mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa IS huko Ar Raqqah, ambako lilipata maendeleo ya kasi kabla ya kukumbwa na upinzani thabiti wa wapiganaji hao.

    Bw. Dillon amesema, jeshi la Marekani linakadiri kuwa hivi sasa wapiganaji elfu mbili wa kundi la IS wapo mjini Ar Raqqah.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako