• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: Duka la Nakumatt Rwanda liko imara licha ya mengine kwenye kanda

  (GMT+08:00) 2017-07-13 18:53:42

  Duka la Nakumatt tawi la Rwanda limeendelea kuwa na matokeo mazuri licha ya kwamba maduka hayo nchini Kenya na Uganda yametumbikia kwenye hasara kubwa huku baadhi yakifungwa.

  Mkurungezi wa duka hilo nchini Rwanda Adam Ramata, amesema kufungwa kwa baadhi ya maduka nchini Kenya na Uganda hakutaathiri oparesheni zake Kigali.

  Ramata alisema Nakumatt Rwanda iko kwenye harakati za kufungua tawi la nne nchini humo ndani ya mwezi mmoja ujao ikiwa mipango yote itafanikiwa.

  Kwa kipindi kvcha mwaka mmoja na nusu uliopita maduka ya Nakumatt yamekuwa yakikabiliwa na kipindi kigumu huku madeni yakizidi dola milioni 170.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako