• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Kenya kununua mashine ya kukagua ubora wa gesi inayotoka Tanzania

  (GMT+08:00) 2017-07-13 18:57:27

  Kenya imetangaza akwamba itanunua mashine mpya ya kukagua ubora wa gesi inayotoka Tanzania kuingia nchini humo.

  Vifaa hivyo vitawekwa kwenye maeneo ya mipakani ili kukagua gesi ya kupikia inayosafirishwa kwa barabara.

  Awali Tanzania imelalamikia Kenya kwamba gesi yake imekuwa ikizuiwa kwenye maenei ya mipaka na hivyo kuathiri biashara.

  Tume ya kuratibu kawi nchini Kenya ERC imesema mashine moja itagharimu kati ya dola $100,000 na $400,000.

  Ndani ya miezi miwili iliopita Kenya imezuia tani 4,000 za gesi ya kupika kutoka Tanzania kuingia Kenya katika kituo cha mpakani cha Namanga.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako