• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gavana wa Benki Kuu ya Russia asema uchumi wa Russia umeanza kukua

    (GMT+08:00) 2017-07-14 08:52:26

    Gavana wa Benki Kuu ya Russia Elvira Nabiullina amesema uchumi wa nchi hiyo uko kwenye kipindi cha mwanzo cha duru mpya ya ongezeko. Akiongea kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu mambo ya fedha uliofanyika jana huko St. Petersburg, gavana huyo amesema uchumi wa Russia umekuwa na mwelekeo sahihi na unatarajiwa kukua kwa asilimia 1.3 hadi 1.8 mwaka huu. Kabla ya hapo rais Vladimir Putin wa nchi hiyo pia alisema takwimu zinaonesha kuwa ongezeko la uwekezaji wa nje nchini Russia limezidi kiwango cha ukuaji wa uchumi, hali inayoonesha kuwa ufufukaji wa uchumi wa Russia umeingia kwenye kipindi kipya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako