• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazitaka pande zote husika za Peninsula ya Korea zifanye juhudi kuhimiza utatuzi wa suala hilo

    (GMT+08:00) 2017-07-14 18:40:46

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesisitiza kuwa, ufumbuzi wa suala la nyuklia la Peninsula ya Korea unategemea juhudi za pamoja za pande zote zinazohusika.

    Habari zinasema ofisa wa Marekani amedai kuwa serikali ya Trump itaziwekea vikwazo vipya benki ndogo za China na kampuni zinazofanya biashara na Korea ya Kaskazini ndani ya wiki kadhaa ijayo.

    Bw. Geng Shuang akijibu maswali kuhusu habari hiyo amesema, China inatekeleza kwa pande zote maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Korea ya Kaskazini huku ikipinga utekelezaji wa vikwazo dhidi ya pande mmoja nje ya mfumo wa Baraza hilo. Katika muda mrefu uliopita, China imekuwa ikichangia katika utatuzi wa suala la Peninsula ya Korea, lakini baada ya kupitishwa kwa uamuzi kuhusu utatuzi wa suala hilo, China itakabiliwa na vikwazo kwa upande wake peke yake, kitendo hiki cha Marekani ni kuvinja daraja baada ya kuvuka mto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako