• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China inapinga Dalai Lama kwenda nchi yoyote kwa hadhi yoyote kufanya shughuli za kuifarakanisha China

  (GMT+08:00) 2017-07-15 17:48:45

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inapinga kithabiti Dalai Lama kwenda nchi yoyote kwa hadhi yoyote kufanya shughuli za kuifarakanisha China, na inaitaka nchi husika ifanye uamuzi sahihi kwenye suala hili.

  Ofisi ya rais wa Botswana juzi ilisema Dalai Lama atazuru nchi hiyo mwezi ujao, na rais wa Botswana atakutana naye. Kuhusu habari hiyo, Bw. Geng Shuang amesema Dalai Lama amefanya shughuli za kuifarakanisha China kwa muda mrefu, na anajaribu kuufanya mkoa wa Xizang ujitenge na China. China inapinga viongozi na maofisa wa nchi yoyote kuwasiliana naye kwa njia yoyote.

  Bw. Geng Shuang amesisitiza kuwa China inaitaka nchi husika iheshimu ufuatiliaji mkuu wa China na kufanya uamuzi sahihi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako