• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raia wa Marekani ahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela nchini Iran kwa tuhuma za ujasusi

    (GMT+08:00) 2017-07-17 10:07:05

    Msemaji wa mamlaka ya sheria nchini Iran Bw Mohseni Ejeje amethibitisha kuwa mahakama ya Iran imemhukumu raia wa Marekani kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la ujasusi.

    Bw Mohseni Ejeje ametangaza habari hiyo kwa njia ya televisheni akisema mtuhumiwa huyo alitumwa na Marekani kukusanya taarifa za kijasusi nchini Iran, na ana haki ya kukata rufaa dhidi ya kesi yake. Bw Ejeje hajataja jina la mtuhumiwa huyo na ni lini alihukumiwa.

    Jana serikali ya Marekani ilitoa mwito wa kuachiwa huru mara moja kwa raia wa Marekani na wa nchi nyingine wanaofungwa nchini Iran kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya usalama wa taifa, na kusema mashtaka hayo sio ya kweli na ni ya kutungwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako