• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: PM - wakati umefika kwa Watanzania kuondokana na nguo zilizotumiwa Mitumba

    (GMT+08:00) 2017-07-17 19:58:05
    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema wakati umefika kwa Watanzania kuondokana na nguo zilizotumiwa kwa sababu ya kuwepo kwa viwanda vingi vya nguo nchini.

    Waziri Mkuu pia amesema kuwa kuwepo kwa viwanda vya nguo kutasaidia wakulima wa pamba kuwa na soko.

    Pia amewataka kupanda pamba kwa wingi ili sekta ya nguo iweze kupata malighafi ya kutosha.

    Majaliwa alisema haya siku ya Jumamosi wakati alipotembelea kampuni ya Namera Group of Industries, ambayo inahusika katika kutengeneza bidhaa za nguo.

    Majaliwa amesema viwanda vya nguo nchini ni hatua ya kumaliza matumizi ya nguo za mtumba, kwa sababu aina mbalimbali za nguo zinzotengezwa nchini bei yake itakuwa nafuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako