Mkataba huu utaona Uganda, ikitumia bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusafirisha mizigo yake.
Uganda inaona gharama ya bandari ya Dar es Salaam ikiwa nafuu na nzuri kwa kusafirisha mizigo yake.
Waziri wa Usafiri wa Uganda bw Bagiire Aggrey alisema jana wakati wa warsha ya kusainiwa kwa mkataba wamelewano, uamuzi huo uko kwa mstari wa mipango yao ya kuboresha biashara ya Waganda ndani na nje ya nchi.
Kulingana na Bagiire, serikali ya Uganda ilipongeza jinsi Tanzania imeboresha bandari ya Dar es Salaam, ambayo inatoa ushirikiano mzuri kwa nchi zengine za Afrika Mashariki.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |