• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kipa wa Manchester City Joe Hart kujiunga na West Ham

  (GMT+08:00) 2017-07-18 10:44:48

  Kipa wa Manchester City na timu ya taifa ya soka ya Uingereza Joe Hart amefanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kukamilisha uamisho kutoka klabu hiyo na kuingia West Ham kwa mkopo.

  Hart aliambiwa anaweza kupata klabu nyingine na meneja wa City, Pep Guardiola baada ya kukaa msimu uliopita katika klabu ya Italia ya Torino.

  Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 ana mkataba na City hadi mwaka 2019 lakini West Ham wana chaguo la kumsajili kwa makubaliano ya kudumu baada ya mkopo huo kukamilika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako