• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Rwanda kuvuna dola milioni 1.8 kutoka kwa kongamano la uwekezaji

    (GMT+08:00) 2017-07-18 20:03:45

    Kongamano la uwekezaji wa sekta ya hoteli nchini Rwanda lililotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu litakusanya franki bilioni 1.5 ama dola milioni 1.8 .

    Kwa mujibu wa ukaguzi wa kifedha nchini humo ,kongamano hilo la siku tatu, litatoa fursa za ajira 1114 pamoja na zaidi ya milioni 247 mapato ya biashara.

    Sekta za utalii na maonyesho zinatarajiwa kuongeza mapato ya dola milioni 400 mwaka huu kufuatia kongamano hilo.

    Halmashauri ya ushuru ya Rwanda imeripoti kwamba idadi kubwa ya fedha katika kongamano la mwaka huu ,itatokana na wajumbe zaidi ya 500 watakaohudhuria kutoka nchi mbali mbali za Afrika.

    Kongamano hili la siku tatu litajadili maendeleo ya uchumi pamoja na miradi ya kubuni ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako