• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda;mashirika ya umma yasisitiza marufuku ya mitumba

    (GMT+08:00) 2017-07-18 20:04:21
    Muungano wa mashirika ya umma ya jumuiya ya Afrika Mashariki, umeunga mkono pendekezo la viongozi wa Afrika Mashariki la kuzuia uingizaji na uuzaji wa nguo za mitumba.

    Faith Lumonya afisa mkuu wa taasisi ya biashara ya Afrika Mashariki amesema ni muhimu kwa marufuku hayo kutekelezwa ili kuiokoa sekta ya viwanda vya nguo.

    Uganda ikiwa ni muathiriwa mkuu wa kudorora kwa sekta ya nguo,marufuku ya biashara ya mitumba itafungua fursa milioni 2.5 za ajira.

    Jijini Kampala biashara hiyo imekita mizizi hivyo kuzuia maendeleo ya biashara ya nguo mpya zinazotengenezwa hapo.

    Mwaka 2015 februari viongozi wa Eac walikubaliana kusitisha biashara ya mitumba jambo ambalo halijatekelezwa hadi sasa.

    George Mugimbi mkurugenzi mkuu wa muungano wa viwanda Uganda ameitaka jumuiya ya EAC kuanza kutekeleza marufuku hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako