• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Marekani kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara

    (GMT+08:00) 2017-07-19 18:50:51

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema tangu China na Marekani kuanzisha uhusiano wa kibalozi miaka 40 iliyopita, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili umewanufaisha watu wao na hata uchumi wa dunia.

    Lu Kang amesema hayo alipozungumzia duru ya kwanza ya mazungumzo ya uchumi ya pande zote kati ya China na Marekani yatakayofanyika leo mjini Washington, Marekani.

    Katika mazungumzo hayo, pande hizo mbili zitafanya majadiliano ya kina kuhusu sera ya uchumi wa jumla, ushirikiano wa biashara na uwekezaji, na utawala wa uchumi duniani. Pia zitatafuta njia ya kupanua ushirikiano na kuondoa maoni tofauti, ili kuuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kupata maendeleo mazuri yenye uwiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako