• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Watalii wa  Poland wanaozuru eneo la milima ya Taita waongezeka.

    (GMT+08:00) 2017-07-19 19:07:26
    Idadi ya watalii wa kutoka Poland wanaozuru eneo la milima ya Taita imeongezeka.

    Sasa watalii wengi wanafika eneo hilo kutokana na kuanzishwa kwa ziara za ndege za moja kwa moja kutoka mji mkuu Warsaw ambazo zilianza kuhudumu mwaka jana .

    Mwaka jana mwezi Juali shirika la ndege la Small Planet Charter lilizanza safari zake kwenda moja kwa moja mjini Mombasa mji ulio karibu na eneo la Taita.

    Shirika hilo linafanya ziara za mara moja kila wiki huku nayo serikali ya Kenya ikiwa imepunguza kodi inazotoza ndege za kukodi ili kukuza utalii.

    Waziri wa utalii wa Kenya Najib Balala amesema ziara hizo zitaendelea hadi mwezi Oktoba.

    Kila wiki ziara hizo kutoka Polanda zinaleta zaidi ya watalii 200 kwenye eneo la pwani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako